• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Yemen anusurika shambulizi la risasi

    (GMT+08:00) 2019-01-18 09:57:06

    Deraya la kijeshi la Umoja wa Mataifa lililokuwa lililom kiongozi wa tume ya umoja huo limeshambuliwa kwa bunduki, na watu wote wako salama.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema shambulizi hilo lilitokea jana wakati kiongozi wa tume ya uratibu ya umoja huo nchini Yemen Bw. Gen Cammaert na maofisa wake wanaondoka baada ya kukutana na serikali ya nchi hiyo. Amesema chanzo cha shambulizi hilo bado hakijulikani, na kutaka pande zote ziheshimu usitishaji vita kwa ajili ya maslahi ya wayemen wote.

    Televisheni ya Al Arabiya inayounga mkono serikali ya Yemen imesema shambulizi hilo limefanywa na kundi la waasi la Houthi, lakini kundi la Houthi limekana kuhusika, na kusema limefanywa na jeshi la serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako