• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China ataka vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi ya Sudan vipitiwe upya

    (GMT+08:00) 2019-01-18 14:23:35

    Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa mataifa Balozi Wu Haitao, amelitaka baraza la usalama la Umoja wa mataifa lipitie upya vikwazo dhidi ya Sudan baada ya hali ya jimbo la Darfur kuboreka.

    Balozi Wu amesema hali ya jumla ya usalama katika jimbo la Darfur ni shwari, na serikali ya nchi hiyo inafanya kazi ya ujenzi na kuinua uwezo kwenye utawala na usalama.

    Amesema baraza la usalama la Umoja wa mataifa linatakiwa kupitia upya vikwazo dhidi ya Sudan kwa wakati, na kufanya marekebisho kwa mujibu wa maendeleo ya sasa, na hatimaye kuondoa vikwazo hivyo.

    Balozi Wu pia ameitaka jumuiya ya kimataifa itoe msaada wa kibinadamu na kiuchumi kwa Sudan, lakini pia amevitaka vyama vya upinzani na makundi yenye silaha kuacha matumizi ya nguvu na kutafuta suluhu kwa njia za kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako