• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yatoa wito kukinga duru ijayo ya kudidimia kwa uchumi

    (GMT+08:00) 2019-01-18 17:10:14

    Naibu mkurugenzi mkuu wa kwanza wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bw. David Lipton amesema, hivi sasa uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto mbalimbali, hivyo nguvu mbalimbali za kiuchumi zinatakiwa kujiandaa mapema iwezekanavyo na kukinga hatari ya duru ijayo ya kudidimia kwa uchumi.

    Bw. Lipton ametoa makala kwenye tovuti IMF ikisema, uzoefu wa kihistoria umeonesha dalili za kudidimia tena kwa uchumi, na kupendekeza nguvu mbalimbali za kiuchumi kutumia sera za sarafu, sera za kifedha na mifumo mbalimbali ya usimamizi iliyozinduliwa baada ya msukosuko wa kifedha kujikinga na hatari hiyo.

    Mbali na hayo, Bw. Lipton pia amesisitiza umuhimu wa kulinda mfumo wa pande nyingi. Amesema, mashirika ya pande nyingi yametoa mchango mkubwa katika kukabiliana na msukosuko na kuhakikisha uendeshaji wa kawaida wa uchumi wa dunia, hivyo ni muhimu kuendelea kuhimiza mchakato wa mageuzi yake ili kukabiliana na changamoto ya uchumi wa ulimwengu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako