• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Majeshi ya Israel na Russia yakubali kuendelea kushirikiana nchini Syria

    (GMT+08:00) 2019-01-18 18:01:04

    Jeshi la ulinzi la Israel limesema limefanya mkutano na ujumbe wa jeshi la Russia na kukubali kuendelea na ushirikiano wao nchini Syria.

    Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo imesema, mkutano huo umefanyika katika mazingira mazuri na ya kitaaluma, na pande hizo mbili zimejadili juu ya kuimarisha mfumo wa kuepuka mgogoro unaoweza kutokea kati ya majeshi ya nchi hizo kaskazini mwa Syria.

    Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amewasiliana kwa simu na rais wa Russia Bw. Vladimir Putin, na kusisitiza kutokomeza ugaidi na kuhimiza kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa na kuimarisha ushirikiano kwa kupitia njia ya kijeshi na kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako