• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zimbabwe yaamuru kampuni nyingine ya huduma za internet ifungwe

    (GMT+08:00) 2019-01-18 18:22:56

    Serikali ya Zimbabwe imeamuru kufungwa kwa kampuni inayotoa huduma za mtandao wa internet kuanzia jana usiku ili kuzuia mawasiliano kati ya waandamanaji wanaopinga kuongezeka kwa bei ya mafuta na kupanda kwa gharama za maisha.

    Mapema leo, kampuni kubwa inayotoa huduma za internet nchini humo Econet imewafahamisha watumiaji wake kuwa serikali imetoa amri nyingine ambayo hawana budi kuifuata. Hatua hii imekuja baada ya kukatika kwa huduma ya internet kwa zaidi ya 24 kati ya jumanne na jumatano wiki hii.

    Hata hivyo, watumiaji wa mtandao wa internet wanaendelea kuwasiliana kupitia mtandao wa kijamii wa 'Whatsapp' na 'Telegram' baada ya kuweka VPN kwenye simu zao za kisasa za mkononi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako