• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yaomba wawekezaji kuisaidia kujenya nyumba za bei nafuu

  (GMT+08:00) 2019-01-18 18:47:27

  Serikali ya Kenya imesema inalenga kuimarisha maeneo ya makazi ya gharama ya chini.

  Kutokana na hilo, imetuma ombi kwa wawekezaji wa kibinafsi kuisaidia katika kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za gharama ya chini nchini.

  Katibu Mkuu wa Nyumba na Maendeleo ya Miji nchini Kenya Charles Hinga amesema wote wanaolenga kushirikiana na serikali wana chini ya mwezi mmoja kutuma maombi.

  Hinga amesema wote wanaolenga kuhusika watatuma maombi kwa kujaza fomu ya kimtandao.

  Kuambatana na mpango huo, serikali inalenga kujenga majumba 1,640 ya orofa Park Road, Starehe (3,500), Shauri Moyo (5,300), Social Housing (15,000) na Mavoko (5,500).

  Kaunti zitakazoshirikishwa katika mpango huo zitanufaishwa na majumba

  48,000 huku Nairobi na Mombasa zikitarajiwa kuwa na majumba mengi zaidi.

  Mpango huo utazinduliwa katika muda wa miaka mitatu ijayo na tayari ekari 7,000 zimetengwa kwa ujenzi huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako