• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump na kiongozi mwandamizi wa Korea Kaskazini kukutana Ikulu ya Marekani

    (GMT+08:00) 2019-01-19 16:50:42

    Rais Donald Trump wa Marekani na makamu mwenyekiti wa kamati kuu ya Chama cha Wafanyakazi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Yong Chol, watakutana ijumaa mchana katika Ikulu ya Marekani.

    Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi Sarah Sanders amesema viongozi hao watajadili masuala ya kuondoa silaha za nyuklia na uhusiano wa pande mbili.

    Mapema jana Bw. Kim alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo, na wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema walikuwa na mazungumzo mazuri. Bw. Pompeo na Bw. Kim walikuwa wanatarajiwa kujadili tarehe na mahali utakapofanyika mkutano wa pili kati ya Rais Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako