• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ailaumu Marekani kutokamilisha mchango wake

    (GMT+08:00) 2019-01-19 16:51:09

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema pengo la asilimia 3 la bajeti ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa lililosababishwa na Marekani, kwa kuzuia mchango wake kwa umoja wa mataifa, halivumiliki.

    Marekani imesema haiwezi kulipa zaidi ya asilimia 25 ya bajeti ya ulinzi wa amani wa umoja wa mataifa, wakati Umoja wa Mataifa umeiagiza kulipa asilimia 28. Bw. Guterres amesema pengo hilo asilimia tatu ni changamoto kubwa kwa umoja wa mataifa, kwa kuwa hawezi kutatua tatizo hilo kwa kubana matumizi kwa asilimia 3.

    Hadi sasa hali imedhibitiwa kwa kuwa pengo hilo linagharamiwa na nchi zinazochangia askari na polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako