• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa viwanda, biashara na ushirikiano wa Kenya asema uwekezaji wa China utahimiza maendeleo ya sekta ya magari nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-01-19 16:53:17

    Kituo cha uendeshaji cha Foton Motor kwenye kanda ya Afrika Mashariki kimezinduliwa jana mjini Nairobi. Kwa niaba ya waziri wa viwanda, biashara na ushirikiano wa Kenya Bw. Peter Munya, Mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa uwekezaji ya Kenya Bw. Moses Ikiara amesema, uwekezaji wa kampuni za China utahimiza maendeleo ya sekta ya magari ya nchi hiyo, na kusaidia kutimiza malengo manne ya maendeleo yaliyotolewa na rais Uhuru Kenyatta.

    Bw. Ikiara amesema kwa mujibu wa malengo manne ya maendeleo, ifikapo mwaka 2022 sekta ya uzalishaji viwandani itachangia asilimia 15 ya ongezeko la uchumi kutoka asilimia 9 ya sasa. Hivi sasa Kenya inategemea kuagiza magari kutoka nje, na asilimia 80 kati ya magari hayo ni mitumba. Kuwekeza kwenye sekta ya magari nchini Kenya kwa kampuni za China, ikiwemo kampuni ya Foton Motor, kutaboresha hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako