• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Cameroon akutana na mjumbe maalumu wa rais wa China

    (GMT+08:00) 2019-01-19 18:50:18

    Rais Paul Biya wa Cameroon jana huko Yaounde alikutana na mjumbe maalumu wa rais wa China Bw. Yang Jiechi, ambaye pia ni mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.

    Bw. Yang amesema lengo la ziara yake ni kuimarisha mawasiliano na Cameroon, kutekeleza maoni ya pamoja yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, kuhimiza utimizaji wa mafanikio ya mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing, na kusukuma mbele ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Cameroon.

    Rais Biya amesema Cameroon inapongeza pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kuunga mkono ushirikiano chini ya mfumo wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako