• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama nchini DRC yathibitisha ushindi wa Tshisekedi kwenye uchaguzi wa Rais wa DRC

    (GMT+08:00) 2019-01-20 17:10:40

    Mahakama ya katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imemthibitisha Bw. Felixi Tshisekedi kuwa mshindi kwenye uchaguzi wa urais, baada ya kukataa pingamizi la kisheria la mgombea aliyepata nafasi ya pili Bw. Martin Fayulu.

    Mahakama imesema Bw Tshisekedi aliyegombea urais kwa tiketi ya chama cha UDPS ni mshindi kwa kupata asilimia 38.5 ya kura, na Bw Martini Fayulu amepata nafasi ya pili kwa kupata asilimia 28 ya kura, na kufuatiwa na mgombea wa chama tawala Bw. Ramazani Shadary.

    Alhamisi Umoja wa Afrika uliitaka tume ya uchaguzi isitangaze matokeo hadi itakapotuma tume yake mjini Kinshasa kuanza mchakato wa kutafuta suluhu ya amani. Msemaji wa serikali Bw Lambert Mende, jana alitoa taarifa akisema mahakama iko huru na inatakiwa kutoa maamuzi kwa mujibu wa ratiba iliyoamuliwa kisheria, licha ya matakwa ya Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako