• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan kuendesha duru nyingine ya mazungumzo ya amani ya CAR wiki ijayo

    (GMT+08:00) 2019-01-20 17:18:34

    Serikali ya Sudan imetangaza kuwa duru nyingine ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi 14 ya upinzani itafanyika wiki ijayo mjini Khartoum, Sudan.

    Waziri wa mambo ya nje ya Sudan Bw. Al-Dirdiri Mohamed Ahmed amesema, serikali ya CAR na makundi ya upinzani yatashiriki kwenye mazungumzo yatakayofanyika wiki ijayo tarehe 24 Januari.

    Mazungumzo hayo yanalenga kushughulikia masuala ya utawala wa serikali, msamaha, wapiganaji kurudi katika jamii na ushiriki wa vyama vya siasa kwenye utawala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako