• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yalaani maadui kujaribu kuvunja uhusiano kati yake na Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-01-20 18:04:07

    Shirika la habari la IRNA la Iran limetoa habari likisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Bahram Qasemi amesema uhusiano kati ya Iran na nchi nyingi za Ulaya zikiwemo nchi tatu zilizosaini makubaliano kuhusu silaha za nyuklia na Iran unakabiliwa na changamoto kutoka kwa maadui.

    Habari kutoka vyombo vya habari vya nchi za nje zinasema kutokana na kidokezo cha Shirika la ujasusi la Marekani CIA, jeshi la Ujerumani lilimkamata mwafghanistan mwenye uraia wa Ujerumani ambaye amewahi kuwa mkalimani wa jeshi la Ujerumani. Habari zinasema, mtu huyo aliwahi kutoa habari kwa idara ya ujasusi ya Iran mara nyingi.

    Bw. Qasemi amesema, mtuhumiwa huyu hana uhusiano na serikali ya Iran, na ni dhahiri kuwa, shutuma hizo zinatolewa na watu wanaojaribu kuvuruga uhusiano kati ya Iran na Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako