• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM alaani shambulizi dhidi ya walinzi wa amani nchini Mali

    (GMT+08:00) 2019-01-21 08:18:04

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vikali shambulizi dhidi ya kambi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa nchini Mali, ambalo limesababisha vifo vya askari kumi wa kulinda amani kutoka Chad.

    Bw. Guterres ametoa wito kwa mamlaka za Mali na makundi yaliyosaini makubaliano ya amani, kufanya juhudi zote kuthibitisha wahusika wa shambulizi hilo na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo. Amesema mashambulizi dhidi ya walinzi wa amani wa Umoja wa mataifa yanachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita, na pia amesisitiza kuwa vitendo kama hivyo havitayumbisha dhamira ya Umoja wa mataifa ya kuwaunga mkono watu na serikali ya Mali.

    Shambulizi hilo lilitokea asubuhi ya Jumapili huko Aguelhok, eneo la Kidal na kusababisha vifo vya askari 10 wa kulinda amani na wengine 25 kujeruhiwa. Baadhi ya washambuliaji pia waliuawa kwenye mapambano na kikosi cha Umoja wa mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako