• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel na Chad zarejesha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-01-21 08:51:55

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema waziri mkuu wa Israel Bw Benjamin Netanyahu na rais Idriss Deby wa Chad wametangaza kurejesha uhusiano wa kibalozi kati ya nchi zao.

    Taarifa hiyo imetolewa baada ya Bw. Netanyahu kufanya ziara ya kwanza nchini Chad mapema jana, ambayo imesema pande zote mbili zinaona kurejesha uhusiano wa kibalozi ni jambo la muhimu kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na maslahi ya pande zote.

    Baada ya ziara yake, Bw. Netanyahu amesema mbali na Chad, Israel itarejesha uhusiano wa kibalozi na nchi nyingine za Kiislam, kitendo ambacho mapinduzi kwenye dunia ya Kiarabu na ya Kiislam, lakini bado hajataja majina ya nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako