• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe akatisha ziara ya Davos na kurudi nyumbani kushughulikia maandamano

    (GMT+08:00) 2019-01-21 08:55:08

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amekatisha ziara yake ya Davos, Uswisi na kurudi nyumbani kushughulikia mvutano unaoendelea kuongezeka nchini Zimbabwe.

    Rais Mnangagwa ametoa ujumbe kupitia Twitter kuwa anarudi nyumbani baada ya mikutano miwili yenye mafanikio kuhusu biashara na uwekezaji. Amesema kwa sasa atawakilishwa na waziri wa Fedha Bw. Mthuli Ncube, na kipaumbele kwa sasa ni kuhakikisha kunakuwa na hali ya utulivu na mambo kuendelea nchini Zimbabwe.

    Nchini Zimbabwe watu wameandamana kupinga ongezeko la bei ya mafuta. Mpaka sasa watu watatu wamekufa kwenye mapambano huku maduka kadhaa yakiporwa na baadhi ya nyumba kubomolewa.

    Rais Mnangagwa ambaye amefanya ziara nchini Russia, Azerbaijan, Belarus na Kazakhstan, alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa Davos unaoanza kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako