• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNRWA yasema uwepo wake huko Jerusalem si "zawadi kutoka Israel"

    (GMT+08:00) 2019-01-21 09:24:21

    Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Palestina UNRWA Bw. Sami Mushasha, amesema uwepo wa shirika hilo huko Jerusalem "si zawadi kutoka Israel", bali ni idhini ya azimio la Umoja wa Mataifa inayoendana na sheria ya kimataifa.

    Ametoa maoni juu ya habari kutoka Israel zinazosema mamlaka zitafunga vituo vya kutoa huduma vya Umoja wa Mataifa katika eneo la mashariki mwa Jerusalem zikiwemo shule kabla ya kuanza kwa muhula ujao wa masomo, na kusema kuwa UNRWA haijapata taarifa yoyote kuhusu jambo hilo. Amesisitiza kuwa shirika hilo litaendelea kutoa huduma kwa wakimbizi wa Palestina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako