• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Erdogan asema Uturuki iko tayari kushughulikia usalama wa Manbij, Syria bila kuchelewa

    (GMT+08:00) 2019-01-21 09:24:45

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Donald Trump na kusema nchi yake iko tayari kushughulikia usalama wa Manbij, Syria bila kuchelewa.

    Kwenye mazungumzo yao ya simu, marais hao wamekubaliana kuongeza kasi ya mazungumzo ya wakuu wa majeshi ya nchi zao kuhusu kuanzishwa eneo la usalama kaskazini mwa Syria. Rais Erdogan amesema shambulizi la bomu lililotokea Alhamisi iliyopita na kusababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani, ni hatua ya uchokozi inayolenga kuizuia Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako