• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Mbio za London: Kipsang atangaza kupigania ubingwa

    (GMT+08:00) 2019-01-21 09:30:26

    Mwanariadha wa Kenya Wilson Kipsang ametangaza kurejea kuwania taji la shindano la riadha la London nchini Uingereza litakalofanyika April 28, 2019.

    Kipsang anajivunia mataji ya mbio za London za mwaka 2012 na 2014 amesema yuko tayari kushindania taji dhidi ya Eliud Kipchoge ambaye anashikilia rekodi ya dunia.

    Kitakuwa kivumbi kikali kwa sababu mbali na Kipchoge, ambaye anajivunia rekodi ya saa 2:01:39 katika mbio za kilomita 42, pia kuna Muethiopia Shura Kitata na Muingereza Mo Farah waliomaliza makala yaliyopita katika nafasi ya pili na tatu.

    Naye mshindi wa mbio za Chicago, Brigid Kosgei ameongezwa katika orodha ya kinadada watakaowania taji hili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako