Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya takwimu ya taifa ya China NBS, zinaonesha kuwa pato la taifa la China GDP limezidi RMB yuan trilioni 90, sawa na dola za kimarekani trilioni 13.24. Uchumi wa China kwa mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 6.6, kiasi ambacho kimezidi lengo la asilimia 6.5 lililowekwa na serikali, na kuwa chini kuliko asilimia 6.8 cha mwaka 2017.
Takwimu hizo pia zimeonesha kuwa, ongezeko la uchumi katika robo ya nne lilikuwa asilimia 6.4, ambalo ni chini kuliko asilimia 6.5 la robo ya tatu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |