• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia pande husika nchini DRC kujitahidi kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-01-21 18:50:06

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inatarajia pande zote husika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo (DRC) kuendelea kujitahidi kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya taifa na kutarajia jamii ya kimataifa kujenga mazingira mazuri kwa jambo hilo.

    Bi Hua amesema, uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita nchini DRC ni jambo muhimu kwa nchi hiyo, na China inampongeza Bw. Felix Tshisekedi kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

    Habari zinasema, marais wa Afrika Kusini, Kenya, Tanzania na Burundi pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC pia zimepongeza ushindi wa Bw. Tshisekedi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako