• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Forodha ya China yapambana vikali biashara haramu ya pembe za ndovu

    (GMT+08:00) 2019-01-21 19:12:50

    Shirika la WildAid na WWF zimetoa tangazo la video la kukinga biashara haramu ya pembe za ndovu, ambalo linawataka watalii wasilete pembe za ndovu na bidhaa za pembe hizo nchini China, ili wasivunje sheria, ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu China kuweka vikwazo vya biashara ya pembe za ndovu.

    Habari zinasema, tangazo hilo litaonyeshwa kwenye forodha za Guangdong, Guangxi, Yunnan, viwanja vya ndege na vituo vya reli katika miji kadhaa ikiwemo Beijing, Shanghai, Guangzhou, na Shenzhen.

    Serikali ya China imeweka vikwazo katika uuzaji na utengekezaji wa bidhaa za pembe za ndovu tangu tarehe Mosi Januari mwaka 2018, na imekuwa nchi inayochukua hatua kali zaidi ya kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako