• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miamala kwa njia ya simu nchini Kenya kwa mwaka jana ilifikia dola bilioni 39.4 licha ya kodi kubwa

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:27:43

    Benki Kuu ya Kenya imetangaza kuwa thamani miamala iliyofanyika kwa njia ya simu nchini Kenya kwa mwaka imeongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 3.4.

    Thamani ya jumla ya miamala kwa mwaka huo ilikuwa dola za kimarekani bilioni 39.4, likiwa ni ongezeko la kutoka dola bilioni 36 za mwaka 2017. Ongezeko hilo limetokea licha ya serikali kuongeza kodi ya miamala kutoka asilimia 10 hadi 12 ya mwaka mwezi Julai, hadi kufikia asilimia 20 ya mwezi Septemba.

    Idadi ya watu walioajiriwa na watoa huduma wa mashirika makubwa matatu ya simu za mkononi pia imeongezeka. Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi pia imeongezeka kutoka milioni 37.4 wa mwaka 2017 na kufikia milioni 47.7 wa mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako