• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafikiria kusaini makubaliano na Sudan Kusini na Ethiopia ili kuhamasishwa uhamiaji wa wahasibu

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:28:13

    Taasisi ya wahasibu ya Kenya (ICPAK) imesema inataka kusaini makubaliano ya kutambuana na Sudan Kusini na Ethiopia, ili kuhimiza uhamiaji wa wahasibu. Akiongea jana mjini Nairobi, mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Julius Mwatu amesema nchi zinazokua haraka kiuchumi katika eneo la Afrika Mashariki, zina mahitaji yanayoongezeka ya wahasibu wenye sifa.

    Bw. Mwatu amesema wanatarajia kusaini makubaliano na taasisi za uhasibu za nchi hizo katika mwaka mmoja unaokuja, ili kuwawezesha wahasibu wa Kenya kufanya kazi katika nchi hizo.

    Bw. Mwatu amesema tayari Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi zimesaini makubaliano ya kutambuana kwenye taaluma ya uhasibu. Amesema kutokana na utandawazi, wafanyakazi wa Kenya wamekuwa wakienda kufanya kazi katika nchi nyingine duniani. Wanachofanya ni kuhakikisha wahasibu wa Kenya wanapata ajira popote wanapotafuta fursa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako