• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio 37 kuhusu watoa misaada ya kibinadamu yalitokea nchini Sudan Kusini katika mwezi December

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:28:34

    Matukio 37 kuhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu yaliripotiwa katika mwezi uliopita nchini Sudan Kusini, mengi yakitokea katika majimbo ya Upper Nile, Jonglei na Equatoria ya kati. Shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limesema asilimia 46 ya matukio hayo yalihusu matumizi ya mabavu dhidi wafanyakazi na mali.

    OCHA imesema kaunti tatu za Rubkoma, Maban na Fangak zilikuwa na matukio mengi zaidi vya vikwazo vilivyohusika na urasimu na vitisho, na unyanyasaji wa wafanyakazi. Matukio kumi yalikuwa makali zaidi, yakihusisha vikwazo vya kiurasimu katika eneo la Sobat, na mgogoro katika maeneo ya Yei na Lainya uliosababisha kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako