• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalum wa UN nchini Yemen awasili Sanaa kwa ajili ya kumaliza mvutano Hodeidah

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:31:12

    Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Bw Martin Griffiths amewasili katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa unaodhibitiwa na waasi ili kumaliza mvutano huko Hodeidah, mji wa bandari wa Bahari Nyekundu.

    Madhumuni ya ziara ya Bw. Griffiths ni kuwahimiza waasi wasimamishe vita na kuondoka Hodeidah kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwezi uliopita huko Stockholm.

    Wakati huo huo, waasi wa madhehebu ya Shia wametoa taarifa wakisema waasi wa Houthi nchini Yemen wamerusha makombora mawili katika kituo cha kijeshi kilichoko maeneo ya Najran na Asir, kusini mwa Saudi Arabia.

    Zaidi ya hayo shambulizi la bomu la kujitoa mhanga dhidi ya kikosi cha Marekani lilitokea mapema jana mkoani Hasakah, kaskazini mashariki mwa Syria, ambalo limefanywa na Kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako