• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wauawa kwenye shambulizi dhidi ya kituo cha kijeshi

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:35:10

    Jeshi la Nigeria limethibitisha kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram walioshambulia kituo cha jeshi kwenye jimbo la Yobe wameuawa, lakini halikutaja idadi ya vifo.

    Jeshi la Nigeria limesema lilipigana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram kwenye mapambano ya zaidi ya saa 2 jumapili jioni wakati wapiganaji hao walikuwa wanashambulia shule ya vikosi maalumu kwenye eneo la Buni Yadi, kilomita 45 kutoka Damaturu, mji mkuu wa jimbo la Yobe.

    Shambulizi hilo limefanywa na kundi la Boko Haram karibu saa 24 kabla ya rais Muhammadu Buhari kutembelea Damaturu kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi mkuu unaofanyika jumatatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako