• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan kufanya ziara nchini Qatar

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:50:24

    Shirika la habari la serikali ya Qatar (QNA) limesema rais Omar al-Bashir wa Sudan anawasili leo mjini Doha kwa ziara.

    Emir wa Qatar Sheikh Hamad Al Thani anatarajiwa kukutana na Bashir kwenye kasri lake kesho na kujadiliana naye kuhusu uhusiano wa nchi mbili na masuala yenye maslahi ya pamoja.

    Ziara ya Rais Bashir huko Doha ni ya kwanza tangu maandamano yaliyotokea mwezi uliopita, kupinga hali mbaya ya kiuchumi na kuongezeka kwa bei ya bidhaa za msingi. Kwa mujibu wa takwimu za serikali za Sudan, watu 26 waliuawa kwenye maandamano hayo yanayotaka kumaliza utawala wake uliodumu kwa miongo mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako