• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi ya utafiti ya Afrika yatoa fedha kwa ajili ya kuhimiza utafiti wa mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2019-01-22 09:50:42

    Akademia ya sayansi za kijamii ya Afrika yenye makao yake mjini Nairobi Kenya imetangaza kutoa dola milioni 1.9 za Marekani kwa ajili ya kuhimiza utafiti kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.

    Watafiti 15 wa Afrika watapewa fedha hizo ili kuwasaidia kufanya tathmini kamili kuhusu jinsi mabadiliko ya hali ya hewa yanavyoathiri maisha ya watu.

    Kwa kushirikiana na wafadhili wa kimataifa, akademia hiyo itatekeleza mpango mpya wa kuhimiza uchunguzi juu ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika bara la Afrika ambalo limeathirika sana na kuongezeka kwa joto.

    Fedha hizo zinalenga kuimarisha uhusiano kati ya utafiti wa sayansi ya hali ya hewa, na hatua za kisera ili kupunguza athari zake kwa sekta za kimkakati za uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako