• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la SportPesa 2019, kipute kuanza leo Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2019-01-22 10:16:10

    Michuano ya Kombe la SportPesa inaanza kutimua vumbi leo jijini Dar es Salaam Tanzania. Michuano hiyo ambayo imekuwa ikivutia umati mkubwa wa mashabiki ukanda wa Afrika Mashariki wiki itashuhudia timu 8 zikishiriki, huku Kenya na Tanzania kila moja ikiwakilishwa na timu nne

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas amesema matayarisho ya michuano hiyo awamu ya tatu yamekamilika.

    Wakati huo huo mchezaji wa zamani wa timu ya Everton ya Uingereza ambaye ni balozi wa klabu hiyo Steven Pienaar anatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam wiki hii pia atafanya mazoezi na timu ya taifa ya ya vijana ya Serengeti Boys inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) U17, michuano itakayofanyika baadaye mwaka huu.

    Yanga ya Tanzania itaanza kutupa karata yake leo kwa kuikaribisha Kariobang Sharks ya Kenya huku Simba ya Tanzania watakutana na AFC Leopards ya Kenya kesho jumatano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako