• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Canada kumwachia huru Bibi Meng Wanzhou mara moja

    (GMT+08:00) 2019-01-22 19:06:59

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China inataka Canada kumwachia huru Bibi Meng Wanzhou mara moja, na kuhakikisha haki na maslahi yake halali.

    Pia amesema China inaitaka Marekani kurekebisha makosa yake, kuondoa amri ya kumkamata Bibi Meng Wanzhou, na kutoitaka Canada kumpeleka rasmi nchini Marekani.

    Bibi Hua Chunying amesema, China kwa mara nyingi imeeleza msimamo wake kuhusu tukio hilo, na kusema hii siyo kesi ya kawaida ya kisheria. Amesema Canada inatumia vibaya mkataba wa kubadilishana wahalifu kati yake na Marekani, na imekiuka usalama, haki na maslahi halali ya raia wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako