• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNDP yaichagua Zambia kuwa nchi ya kielelezo ya malengo ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2019-01-22 19:20:52

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mipango ya maendeleo UNDP limeichagua Zambia kuwa moja ya nchi 60 za kielelezo kwa ajili ya Maabara ya Kuchochea Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), pendekezo linalolenga kuhimiza mafanikio ya maendeleo hayo.

    Mkurugenzi wa UNDP wa kanda ya Afrika Bi. Ahunna Eziakonwa amesema hayo alipokutana na waziri wa mipango ya maendeleo ya Zambia Bw. Alexander Chiteme, kando ya mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu Kuibuka kwa Afrika uliofanyika mjini Dakar, Senegal. Amesema Zambia ni moja ya nchi za mwanzo kuhimiza mkakati wa mendeleo ya sekta binafsi unaendana na mahitaji halisi ya nchi hiyo. Pia amemhakikishia Bw. Chiteme uungaji mkono wa shirika lake katika kutimiza ajenda ya maendeleo ya Zambia.

    Kwa upande wake, Bw. Chiteme ametoa wito wa kuendeleza uratibu kati ya Zambia na UNDP, akisema nchi yake imeweka karibu asilimia 86 ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa kwenye mpango wa maendeleo wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako