• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kiwanda kipya cha kahawa kujengwa Embu

  (GMT+08:00) 2019-01-22 19:42:31

  Wakulima wa kahawa katika Kaunti ya Embu huenda wakapata afueni baada ya kiwanda kitakachonunua kahawa moja kwa moja kutoka kwao,kujengwa.

  Kiwanda hicho kitaondoa madalali ambao wamekuwa wakinunua kahawa kutoka kwa wakulima kwa bei duni.

  Kiwanda hicho kinachojengwa kupitia ufadhili wa serikali ya kaunti na vyama vya ushirika vya wakulima, kinatarajiwa kukamilika mwezi ujao.

  Gavana wa Embu Martin Wambora alisema kuwa wakulima watauza mazao yao kwa Sh100 kwa kilo ya kahawa.

  Gavana Wambora alisema kuwa kaunti ya Embu ndiyo huzalisha kahawa ya ubora wa juu zaidi nchini ilhali wakulima wanaendelea kuhangaika kwa kuuza mazao yao kwa bei duni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako