• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan: Waziri mkuu wa Sudan afungua masoko ya vijana

  (GMT+08:00) 2019-01-22 19:43:27

  Waziri mkuu wa Sudan Mutaz Musa amefungua masoko ya vijana kama sehemu ya mipango ya kijamii ya kutatua mzozo wa kiuchumi na kupunguza bei ya bidhaa za kimsingi.

  Kumekuwa na maandamano nchini humo wananchi wakitaka kupunguzwa kwa bei ya mkate.

  Masoko hayo ya vijana yatauza bidhaa kwa bei ya viwandani.

  Waziri wa viwanda na biashara Ja'far Ahmed Abdalla amesema masoko hayo yatasaidia kupunguza gharama ya masiaha na mzozo uliopo kwa sasa.

  Alisema yatasaidia kuongeza ushindani na kupunguza ukiritimba wa wafanyabishara wanaopandisha bei kiholela.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako