• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Kenya bado haijaweza kusafirisha mafuta yake nje ya nchi kama ilivyopangwa

  (GMT+08:00) 2019-01-22 19:45:15

  Mpango wa Kenya wa kuuza nje mafuta yasiyosafishwa, bado hauwezekani, baada ya kampuni ya mafuta ya Tullow kuhahirisha mpango wa usafirishaji wa kwanza hadi Juni.

  Mpango wa kuanza kuuza mafuta ulizinduliwa mwezi Juni 2018, ukilenga kusafirisha mapipa 400,000 mwezi Februari mwaka huu.

  Kampuni hiyo ya mafuta ya Uingereza imesema kuwa tarehe mpya imetolewa baada ya kushindwa kufikia lengo la kupata mapipa 2,000 kila siku kutoka kwenye mashamba ya mafuta huko Lokichar kaskazini-magharibi mwa Kenya.

  Hadi sasa ni mapipa 60,000 tu yamepelekwa kwenye kiwanda cha usafishaji kilichoko Changamwe, pwani ya Kenya.

  Katika taarifa yake ya hivi karibuni ya biashara Tullow ilisema usafirishaji wa mafuta yasiyosafishwa kutoka Turkana kwenda Mombasa kwa barabara unaendelea wastani wa malori nane baa ya kila siku mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako