• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wakulima Tanzania wajitahidi kutosheleza mahitaji ya soko

  (GMT+08:00) 2019-01-22 19:57:24

  Taasisi ya wakulima wa mboga, matunda na maua Tanzania, (Taha), imeweka bayana mwelekeo wa utendaji wa kazi kwa mwaka 2019, huku ikidhamiria kutosheleza soko la ndani la bidhaa zake na kufikia masoko ya kikanda, Afrika na Ulaya.

  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taha, Jackline Mkindi, amsema mwaka jana licha ya kuwapo kwa changamoto mbalimbali, sekta ya kilimo ilikuwa na wawekezaji waliweza kupata masoko hasa katika masoko ya kikanda na kimataifa.

  Aliongeza kuwa ripoti ya East African Trade and Investiment ya mwaka jana, imeonyesha mauzo katika masoko ya kikanda yameendelea kuongezeka sana.

  Alisema kwa mfano, mwaka jana mauzo hayo yaliongezeka kwa asilimia 11, wakati mwaka juzi Tanzania iliuza mazao katika soko la kikanda yenye thamani ya dola laki 6 milioni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako