• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yaongeza uzalishaji wa mafuta mapipa elfu 70 kwa siku

    (GMT+08:00) 2019-01-23 08:54:09

    Waziri wa mafuta wa Sudan Kusini Bw. Ezekiel Lul Gatkuoth amesema Sudan kusini itaongeza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa elfu 70 kwa siku kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Akiongea kupitia taarifa Bw. Gatkuoth amesema visima vya mafuta vya Unity na Toma Kusini vilivyofunguliwa hivi karibuni, vinazalisha mapipa elfu 35 kwa siku, kiasi ambacho kinatarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

    Kwa mujibu wa Benki ya dunia, Sudan Kusini ni nchi inayotegemea zaidi sekta ya mafuta, inayochangia asilimia 60 ya pato la ndani la taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako