• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasimamizi wa makubaliano ya kusimamisha vita Sudan Kusini walalamikia ukosefu wa fedha

    (GMT+08:00) 2019-01-23 09:11:33

    Wasimamizi wa usimamishaji vita Sudan Kusini wamelalamikia ukosefu wa fedha unafanya usimamizi wa utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha vita iliyokuwepo kwa miaka mitano uende polepole.

    Akiongea na wanahabari mjini Juba, mkuu wa tume ya usimamizi Bw. Desta Abiche Ageno, amesema mpaka sasa bado hawajatuma tume ya kitaifa ambayo kazi yake ni kujenga hali ya kuaminiana kwenye ngazi ya mashina, kutokana na ukosefu wa fedha.

    Hata hivyo amesema tume yake inashirikiana na serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa na pande nyingine, kuangalia uwezekano wote wa kutatua changamoto hiyo.

    Amesema kwa sasa tume yake inashindwa kwenda katika baadhi ya sehemu za Sudan Kusini, lakini anaamini kuwa kutokana na ushirikiano utekelezaji wa usimamishaji vita wa kudumu na mipango ya usalama ya mpito, vitachangia usalama na utulivu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako