• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji Kenya wataka kuwe na mageuzi ya kisera ya kuhimiza biashara ya ndani barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-01-23 09:11:57

    Mwito umetolewa kwa serikali za nchi za Afrika kutoa kipaumbele kwenye mageuzi ya sera na sheria ili kuhimiza biashara ya kuvuka mipaka ambayo ni muhimu katika kuleta ongezeko shirikishi la uchumi.

    Mwito huo umetolewa na wajumbe wa shirikisho la Sekta binafsi ya Kenya, wakitangaza tarehe ya mkutano wa saba wa wakuu wa makampuni unaopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Machi mjini Kigali.

    Naibu Mkuu wa shirikisho la Sekta binafsi la Kenya Bw. Rachel Muthoga amesema sekta binafsi inaweza kunufaika na mageuzi ya soko yanayoendelea, kuhimiza biashara ya ndani barani Afrika, na kuchochea ongezeko la uchumi barani Afrika.

    Amesema kuwa na vyanzo mbalimbali vya uchumi kutoka sekta ya kilimo peke yake na kuwa na sekta ya huduma ya fedha na Tehama, kunatakiwa kuwa mkazo mkuu kwenye eneo la biashara huria la Afrika. Shirikisho hilo pia limeunga mkono mageuzi yanayolenga kuhimiza mawasiliano ya kisoko barani na nje ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako