• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China kuisaidia Ghana kuendeleza raslimali za misitu

    (GMT+08:00) 2019-01-23 09:27:58

    Kampuni ya uagizaji na uuzaji wa vifaa vya kielektroniki ya China (CEIEC) na kamati ya misitu ya Ghana wamesaini hati ya maelewano kuhusu kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza raslimali za misitu.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo Ghana na China zitaanzisha mradi wa ushirikiano wa misitu, kuendeleza kwa pamoja uhifadhi wa misitu, na kuisaidia Ghana kunufaika zaidi na raslimali za misitu.

    Naibu mkurugenzi wa kampuni ya CEIEC Bw. Liu Zhirong amesema, ushirikiano huo utaisaidia Ghana kutumia vizuri raslimali za misitu kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wake kwa njia mbalimbali.

    Mamlaka ya misitu Ghana imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na kuzingatia zaidi faida ya muda mfupi, ukosefu wa maendeleo endelevu, ukataji miti usio na mpango, na ukosefu wa teknolojia na vifaa vya kuchakata mbao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako