• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini atoa mwito wa kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2019-01-23 09:28:33

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa mwito wa kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe. Rais Ramaphosa amesema hayo kwenye mkutano wa Shirika la kimataifa la wafanyakazi nchini Uswisi uliofanyika kabla ya Baraza la Uchumi Duniani WEF.

    Rais Ramaphosa amesema Zimbabwe imejiondoa kutoka kwenye hali ngumu ya kisiasa, na pia ilifanya uchaguzi kwa mafanikio hivi karibuni, lakini nchi nyingi duniani bado zimeiwekea vikwazo nchi hiyo.

    Rais Ramaphosa ameitaka jumuiya ya kimataifa ipunguze au kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe, ili iweze kuboresha usimamizi wa uchumi.

    Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bibi Lindiwe Sisulu amesema kuna makampuni ya Afrika Kusini yaliyowekeza nchini Zimbabwe, ambayo yanaathirika kutokana na vikwazo hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako