• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan afanya ziara Qatar

    (GMT+08:00) 2019-01-23 09:36:34

    Rais Omar al-Bashir amewasili Doha na kuanza ziara ya siku mbili nchini Qatar, ikiwa ni ziara ya kwanza nje ya nchi tangu maandamano ya ndani yanayomtaka aondoke madarakani yatokee katika mwezi mmoja uliopita.

    Shirika la habari la Qatar QNA limesema, rais al-Bashir alipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hamad na waziri wa mambo ya nje ya Qatar Bw. Soltan Al-Muraikhi.

    Shirika hilo pia limesema kiongozi wa Qatar Bw. Tamin bin Hamad Al Thani anatarajiwa kukutana na rais al-Bashir na kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala ya maslahi ya pamoja.

    Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Sudan, watu 26 wameuawa katika maandamano hayo yanayotoa wito kumaliza utawala wa rais al-Bashir uliodumu kwa karibu miaka 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako