• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM amteua balozi mpya katika eneo la maziwa makuu

    (GMT+08:00) 2019-01-23 09:47:06

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antionio Guterres ametangaza kumteua Bw. Huang Xia wa China kuwa balozi wake maalumu katika eneo la Maziwa makuu.

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema, Bw. Xia anamrithi Bw. Said Djinnit kutoka Algeria ambaye katibu mkuu amemshukuru kwa huduma zake bora na kazi nzuri katika Umoja wa Mataifa.

    Bw. Xia ana uzoefu wa kidiplomasia wa zaidi ya miaka 30 kote duniani, na kuwa na nyadhifa mbalimbali za ngazi ya juu barani Afrika. Alikuwa balozi wa China nchini Niger kati ya mwaka 2009 hadi 2012, nchini Senegal mwaka 2012 hadi 2015 na nchini Jamhuri ya Kongo mwaka 2015 hadi 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako