• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika walaani shambulizi dhidi ya askari wa Amani nchini Mali

    (GMT+08:00) 2019-01-23 11:03:43

    Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat amelaani shambulizi lililotokea jumapili iliyopita huko Aguelhok, katika eneo la Kidal nchini Mali na kusababisha vifo vya walinzi amani 10 kutoka Chad wa Tume ya kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), na wengine zaidi ya 25 kujeruhiwa.

    Akitoa salamu za rambirambi kwa serikali ya Chad na familia za wafiwa, Bw. Mahmat amewahimiza serikaki ya Mali na makundi yenye silaha yaliyosaini makubaliano ya amani wafanye kila juhudi kuwatambua na kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

    Bw. Faki pia amesisitiza uungaji mkono wa Umoja wa Afrika kwa serikali ya Mali kwenye juhudi za kuleta amani ya kudumu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako