• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawasaidia maveterani kupata kazi

    (GMT+08:00) 2019-01-23 18:54:15

    China imechukua hatua kadhaa kuwasaidia maveterani wake kupata kazi na kulinda haki zao halali na matakwa yao.

    Wizara inayoshughulikia masuala ya maveterani imesema, serikali za mitaa zimewapatia kazi za kawaida zaidi ya wanajeshi wa zamani elfu 80, na kuwasaidia askari wengine laki 4 kurejea katika jamii baada ya kustaafu mwaka jana. Zaidi ya hayo, kampuni 123 za China zinazomilikiwa na serikali zimeungana na kutoa karibu nafasi elfu 15 za ajira kwa maveterani kwa mwaka jana.

    Wizara hiyo imeimarisha elimu na mafunzo kwa maveterani ili kuwafanya wawe na ushindani zaidi katika soko la ajira na kutoa msaada zaidi kwa wanaotafuta kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako