• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongeza uteuzi wa Xia Huang kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Maziwa Makuu

    (GMT+08:00) 2019-01-23 19:03:36

    China imempongeza aliyekuwa balozi wa nchi hiyo nchini Jamhuri ya Kongo Bw. Xia Huang kuwa mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Maziwa Makuu.

    Akizungumzia uteuzi huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Hua Chunying amesema, China inaamini Bw. Xia Huang atatoa mchango kwa ajili ya kuhimiza Umoja wa Mataifa kuunga mkono kanda ya Maziwa Makuu kutimiza amani, utulivu na maendeleo. Amesema, kwa muda mrefu Bw. Xia Huang ameshughulikia mambo ya Afrika kwa kina, na anajua vizuri masuala ya kanda hiyo. China itaunga mkono juhudi za Bw. Antonio Guterres na Bw. Xia Huang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako