• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia kuongezeka kwa idadi ya watu licha ya kupungua kwa watoto wanaozaliwa

    (GMT+08:00) 2019-01-23 19:06:23

    China inatarajia kuongezeka kwa idadi ya watu katika siku zijazo, licha ya kupungua kwa wajawazito.

    Mkuu wa idara ya takwimu ya idadi ya watu na ajira iliyo chini ya Mamlaka ya Taifa ya Takwimu Li Xiru amesema, idadi ya watoto wanaozaliwa itaendelea kupungua kila mwaka kwa muda fulani katika siku zijazo, lakini bado itakuwa juu zaidi ya idadi ya vifo, na China ina karibu wanawake milioni 100 walio kwenye umri wa kupata ujauzito.

    Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka jana, idadi ya watu China imefikia bilioni 1.39, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 5.3 ikilinganishwa na mwaka 2017, huku idadi ya watoto waliozaliwa ikifikia milioni 15.23 mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako