• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa dunia kukua kwa asilimia 3.5 yasema IMF

  (GMT+08:00) 2019-01-23 19:49:02

  Shirika la fedha la kimataifa IMF limetangaza kuwa ukuaji wa kiuchumi duniani unatarajiwa kuwa asilimia 3.5 kwa mwaka huu wa 2019 na sio makadirio ya awali ya asilimia 3.7.

  IMF inasema kupungua kwa matarajio kunachangiwa na masharti magumu kwenye sekta ya fedha, mizoz ya kibiashara na taharuki ya kusubiri kujiondoa kwa Uingereza kutoka kwa Umoja wa Ulaya.

  Kulinga na ripoti ya IMF iliotolewa kwenye mkutano wa kiuchumi duniani huko Davos ukuaji wan chi za kusini mwa jangwa la sahara unatarajiwa kuwa asilimia 3.5 mwaka 2019 ikilinganishwa na asilimia 2.9 ya mwaka 2018.

  Na mwaka 2010 IMF inasema kanda hiyo itakuwa na ukuaji wa asilimia 3.6

  Mkurungezi wa IMF bibi Christine Lagarde, anazishauri nchi mbalimbali kujiepusha na madeni akisema hiyo ndio sababu moja ya kupungua kwa uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako