• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Zaidi ya watu 4,000 wakosa usafiri kisiwani Kyotera

  (GMT+08:00) 2019-01-23 19:49:21

  Zaidi ya watu 4,000 wamekwama kwenye kisiwa cha Kyotera nchini Uganda kutokana na ukosefu wa boti za kuwasafirisha.

  Biashara kwenye vituo vya Kasensero na Kakuuto pia zimekwamba kutokana na tatizo hilo.

  Uchukuzi uliathirika tangu Mei 2018 baada ya polisi wa idara ya uvuvi kuharibu boti za mbao ambazo wenyeji hutumia kusafiri.

  Huduma za matibabu na nyingine za kibiashara kwenye kisiwa hicho cha karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania zimezorota kwa miezi 7 sasa na wakaazi wanalazimika kutafuta huduma nchini Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako