• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mobius yaapata wateja zaidi baada ya kufungua kiwanda kipya

    (GMT+08:00) 2019-01-23 19:50:02

    Kampuni ya kutengeza magari nchini Kenya Mobius Motors imesema zaidi ya magari 300 yameagizwa kabla ya kuanza kutengenezwa kwenye kiwanda chake kipya mjini Nairobi.

    Kiwanda hicho kimejengw kwa gharama ya sjhilingi milioni 500.

    Msemaji wa mmoja wa wadau kwenye kampuni hiyo, Darshan Chandaria, amesema kiwanda hicho kitakuwa na shughuli nyingi ndani ya miezi 14 ijayo ili kutengeneza magari hayo.

    Amesema walitarajia kuwa uagizaji wa magari hayo mapya ya Mobius II utakuwa 100 tu lakini ongezeko la 200 imekuwa ni ishara ya imani ya wakenya kwenye gari hilo.

    Kampuni ya Mobius ilianzishwa mwaka 2009 na mjasiriamali wa Uingereza Joel Jackson, na sasa inatengeneza aina tatu ya magari ghali zaidi likiwa ni dola 15,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako